Thursday, April 8, 2010

Wenger ah unaniboa



Mh uliniuzi ila nakukubali kuwa haufai, umetuonyesha kuwa kuna watoto na mitoto katika soka



Mafans wa Arsenal tumekumiss sana Broza Henry.

Lilikuwa ni jambo la kukubali tu kwamba Barcelona ni wakali kuliko arsenal.Wamewazidi kila kitu kuanzia mbinu, uwezo na utaratibu tu wa uchezaji.. mbaya zaidi Messi alikuwa zaidi ya mchezaji katika game hiyo na zaidi ya mchezaji katika dunia hii.

Aliweza kuamua game yeye peke yake kwa kufunga mabao 4, lakini liko wapi suala la Arsenal Wenger, kocha wa Arsenal kuendelea na sera zake za kuwabeba vijana?me naona wenger anachokosea ni kushindwa kutofautisha kitu "Umri" na vipaji. Arsenal ikifungwa tu utasikia timu ni changa, ina vijana wengi, angalia kiungo kuna avarage ya miaka 21" hii bwana haisaidi kitu unazidi kutuumiza wapenzi na mashabiki wa The Gunners wenye kiu ya kuliona kombe baada ya kulikosa kwa miaka kenda.

Wenger umesahau kwamba timu zingine zina vijana wengi tu wa umri mdogo kama hao makinda wako, lakini wenzetu wana vipaji ndo mana pale, sio umri tu uliowaweka kwenye timu zao. Angalia Sturridge wa Chelse, kijana mdooogo kabisa, Messi aliyekutia aibu ni kijivulana tu, Raphaeli wa man kakijivulana tu, Pagto wa AC Milan, na wengine kibao vijivulana tu lakini vipaji wanavyo. Sipingi kwamba unao vijana wenye vipaji hapo lakini walipaswa kuchanganywa na waongozaji kuwapa mbinu za kusaka ushindi mambo yanapokuwa magumu. Msimu huu ukiondoa Liverpool iliyo hoi bin taaban, hujaifunga timu yoyote kubwa si kwenye ligi kuu wala champions ligi.

Umepigwa na Man nyumbani na ugenini tena vipigo vya aibu. Umepigwa na chelsea home and away, Man city kakulamba, barcelona ndo hivyo, sasa timu gani unayoiita bora kama uzitandiki timu kubwa, maana kipimo cha ubora wa timu imara ni kuzichapa timu kubwa.

Ningekuwa mimi ndo wewe Wenger ningenunua wachezaji wanne tu walio tayari sio watoto yaani kiungo mzuiaji mmoja wa ukweli (Melo), Mshambuliaji mmoja wa ukweli (Higuan ama Dzeko), beki wa kati mmmoja wa ukweli (Hangaland) na kipa yeyote kutoka ulaya ya mashariki. Aaah unaniboa Wenger hata kunenepa sinenepi mwenzio cuz of your team, nunua bwana wenye uwezo msimu ujao tufanye mambo na Messi asituchezee tena.

No comments:

Post a Comment