Tuesday, April 20, 2010

MMOJA AFA, 19 HOI KWENYE AJALI MBAYA ILIYOTOKEA LEO WILAYANI MWANGA,

MTU mmoja amefariki dunia papohapo na wengine 19 kujeruhiwa vibaya baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori katika eneo la daraja la mto kifaru wilayani mwanga mkoani Kilimanjaro.

Ajali hiyo iliyolihusisha gari la Rombo Express lenye namba za usajili T255 AHV lililokuwa likitokea Rombo kwenda jijini Dar es salaam na Lori lenye namba za usajili T754 AEZ lililokuwa likitoke Hedaru wilayani Same kuja Moshi imetokea LEO majira ya saa mbili na nusu asubuhi.Kutokana na ajali hiyo magari yaliyokuwa yakielekea jijini Dar es salaa na Moshi yamelazimika kusimama na kusababisha foleni kubwa kwa muda wa masaa manne .

Akizungumza katika eneo la tukio kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Lucas Ng’hoboko alisema majeruhi wamelazwa katika hospitali ya Mawenzi na KCMC na kwamba aliyefariki ni fundi mitambo wa lori ambapo jina lake bado halijafahamika.

Kamanda Ng’hoboko alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa Lori ambalo lilikuwa limebeba mitambo ya kutengenezea barabara na kwamba uchunguzi unaendelea na pindi utakapokamilika sheria itachukua mkondo wake.

Basi la Rombo express likiwa chali kando ya barabara

mamia ya wakazi wa Kifaru wilayani mwanga wakishuhudia shughuli za uokoaji

Basi la Rombo express

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Lucas Ng'obhoko akizungumza na waandishi wa habari juu ya tukio hilo.

hili ni Lori lilogongana uso kwa uso na basi la Rombo express

Ilikuwa hatari, Poleni wafiwa, na majeruhi mungu atawaafu.AMEN


Ajali hiyo ilisababisha foleni kuuuubwa kwa takribani masaa manne

No comments:

Post a Comment