Monday, April 5, 2010

KASA YAIPIGA JEKI KILI MEDIA FOOTBALL CLUB


Ndo ndo ndo si chururu, kidogokidogo ndiyo mwendo, najua mwanzo mgumu, na kawia ufike.... jamani nawataarifu waandishi wa habari wa Mkoa wa Kilimanjaro wamepania kufanya mageuzi kwenye sekta ya michezo kwa kuanzisha timu za mpira wa miguu na mpira wa pete.

Lengo ni kurekebisha afya zao, kuleta mshikamano na umoja miongoni mwao baada awali Chama chao cha MECKI kukaribia kuwavunja shingo pamoja na kunenga uhusiano wa kimichezo na kijamii baina yao na makundi mengine ya jamii yaliyojiingiza katyika michezo.

Kwa upande wa timu ya mpira wa miguu,KILIMANJARO MEDIA FOOTBALL CLUB, hata kabla ya kuanza mazoezi, tayari wafadhili wameanza kuona uelekeo, tayari shirika moja lisilo la kiserikali linalojihusisha na mapambano dhidi ya Ukimwi kilimanjaro , KASA limeipiga jeki kwa kupatiwa vifaa vya michezo zikiwemo jezi na mipira... ama kweli "Nyota njema uonekana asubuhi"

Cheki hapa



Kaimu katibu wa Kilimanjaro Media Football Club, Nakajumo James akipokea jezi kwa niaba ya timu hiyo kutoka kwa kaimu mwenyekiti wa baraza la wazee Kilimanjaro, Ablallah kimweri, aliyekabidhi kwa niaba ya Mkurugenzi wa KASA, Faraji Swai..



Sio duaa ila ni shukurani toka kwa Nakajumo kwa niaba ya timu kwenda kwa vigogo wa KASA.


Hapa Nakajumo akimkabidhi jezi nahodha wa Kilimanjaro media football club, Dixon Busagaga, aliyepokea kwa niaba ya wachezaji wenzake.




Ziko poa.. kisimba simba..teh teh ila safi....hawa ni baadhi ya wachezaji wa timu hiyo, wakiwa katika uzi waliokabidhiwa na KASA... kutoka kushoto ni Rodrick Mushi, Nakajumo, Busagaga, Kija na Zephania



Tehe teh aapa wapo katika pozi jingine, bila shaka pozi hili ni ubunifu wa Naka.. ila kiukweli jezi ziko poa sana, kazi kwao.

4 comments:

  1. mjomba..naona Clever amekua mfadhili wa vilabu vya moshi..hahahahah...inabidi aanzishe timu sasa..

    ReplyDelete
  2. bwana we sifuni najipanga kuwa Tenga wa baadae ,wengine si wamewahi kutaka kuwa JK,mie nimeona huku kwa Tenga hatuko wengi ngoja tujipange zaidi nahitaji support yenu tu wadau...

    ReplyDelete
  3. hahahah....sawa bwana kila la heri mkuu..ngoja tujipange tuje tuanzishe timu hapo..

    ReplyDelete
  4. sasa hawa jamaa mbona hawafanani na fani,ukimuondoa huyo dj clever:dah mbona wamechoka hivi,au ndio ugumu wa kuuandaa vipindi na kusaka habari?ila kimaukweli kabisa sura zao kama walevi wa gongo vile,mtazamo tu washikaji msijinge chuki.

    ReplyDelete