Friday, April 30, 2010

BUNGE LA CHUO KIKUU HURIA LAFUNGILIWA LEO KILIMANJARO


Mgeni rasmi,mshauri wa maendelo ya jamii mkoa wa kilimanjaro,Paul shayo katikati, akiwa na vigogo wa chuo kikuu huria..kulia ni naibu mkuu wa chuo hicho taaluma,Profesa Elifas Bisanda.

Mziray, watu wa soka wanamfahamu sana huyu jamaa, mpaka timu ya taifa kafundisha,vigogo simba na yanga kafundisha, kwa sasa anatoa darasa kwa madenti wa Chuo kikuu Huria, pia alikuwepo.

Mazimu(blogger) nikimpa kampani ya msosi Rodrick makundi(mwandishi wa magazeti ya uhuru na mzalendo)...me nilikuwa nimeshiba ingawa nilikula kidogooooo, makundi yeye mh alitandika kisawasawa.

Mmoja wa wabunge wa bunge la wanafunzi wa Chuo Kikuu Huria(OUT)akichangia hoja...bunge hilo limefunguliwa na mshauri wa mkoa wa Kilimanjaro wa masuala maendelo ya jamii,Paul shayo kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Monica Mbega.
Mkurugenzi wa mawasiliano na masoko wa Chuo Kikuu Huria, kulia akinielezea jambo(mazimu) kuhusu hizo computer...eti zimeletwa 10 kwenye kituo cha Kilimanjaro, ambazo zitarahisisha usomaji kwa wanafunzi wa chuo hicho.

BANZA AHAMISHIA KIPAJI KWENYE TAARABU.


Ramadhani Ally hassan Mahono Masanja "Bnza Stone"

Kulia Juma(Promota),Mazimu na Banza

Mwanamuzi wa miondoko wa dansi nchini, Banza Stone ameshusha bonge la dude la taarabu ambapo kwa mara ya kwanza limeanza kusikika leo katika radio station mbalimbali nchini. wimbo huo unaitwa "kuzaliwa mjini sina tabu"uliorekodia katika studio za Soundacrafters jijini dar es salaam.

Kwa mujibu wa Banza wimbo huo umetungwa na Thabiti Abdul "mtoto wa Ilala"na kuitikiwa na waimbaji wa TOT taarabu.
Haya Banza karibu katika anga za vidole juuuuuuuuuuuuuu.

TBL ILIVYOIMWAGIA PESA TIMU YA MKOA WA KILIMANJARO KWA AJILI YA TAIFA CUP


Kaimu meneja mauzo wa TBL Kilimanjaro/Tanga, Edmund Rutaraka akikabidhi sh. mil 1.5 kwa niaba ya kampuni yake kwa kaimu mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Hassan Bendeyo ambaye ni Katibu Tawala msaidizi huduma za miundo mbinu, aliyepokea fedha hizo kwa niaba ya chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro,KRFA.

Rutaraka akitoa neno baada ya kukabidhi fedhA hizo kwa Bendeyeko ambaye pia aliwakabidhi viongozi wa KRFA, kulia ni katibu wa KRFA, Benedict Macha,akifuatiwa na makamu mwenyekiti wa chama hicho, Darab Darab.

Mweka hazina wa KRFA, Kusianga Kyata,akihesabu noti za TBl baada ya kukabidhiwa na katibu wake, Macha kwa ajili ya maandalizi ya timu ya mkoa kwenye KILI taifa Cup.
Kusi akichekelea jambo,na Darab

Viongozi wa KRFA,Macha,Kusi, Darab wakizungumza na Mtangazaji na mtayarishaji wa kipindi cha michezo cha radio moshi fm, dixon busagaga.

DIWANI ATIMULIWA KWENYE BARAZA MOSHI.

Diwani wa kata ya Mji mpya, mjini Moshi, Abuu shayo amesimamishwa vikao vitatu vya baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo, baada ya kile kinachodaiwa kukiuka taratibu za kikao....
Kisa ni ishu ya Kugaiwa kwa eneo la uhuru Park kwa kampuni ya Tanzania Discover Heritage, iliyotaka hati ya eneo hilo kwa mkataba w amiaka 33 ili ikakope pesa bil 1.5 za kuliendeleza.Kati ya madiwani 22 waliohudhuria kikao cha march 31 mwaka huu kupitisha uamuzi wa kumpa mwekezaji huo, madiwani 6 waligoma akiwemo Abuu ambaye ni diwani kwa tiketi ya CHADENA.

Sasa bwana katika kikao cha juzi kubatilisha uamuzi huo, ilikuwa kasheshe...hawa wanataka wawajibishwe baadhi ya watu, hawa wanataka kuendelea kumwaga sifa za kilichofanywa na CCM..mwisho wa siku yakamkuta Abuu kama haya..

Diwani wa kata ya Mji Mpya manispaa ya Moshi Abuu Shayo akiimba tumeshinda!Tumeshinda baada ya kubatilishwa azinio lakutolewa kwa hati usu kwa mwekezaji wa Uhuru Park ili aweze kukopa kiasi cha shilingi bilion 1.5 .

Madiwani wa Chadema wakijadilina baada ya kutoka nje ya kikao cha baraza la madiwani wakipinga Meya kuruhusu kujadiliwa hoja ntyingine tofauti na ile ya Uhuru Park.

Abuu Shayo".hatuwezi kuendelea na hoja ya mafanikio sisi tutajadili uhuru park pekee".

Diwani Jafary ."endeleeni na kikao chenu cha hoja ya mafanikio"

Thursday, April 29, 2010

TID& KIBA LIVE IN LONDON THIS FRIDAY

Mwanamuziki TID na mwenzake Ally kiba wako nchini Uingereza katika jiji la London, ambapo april 30 mwaka huu wanafanya bonge la show katika ukumbi wa CLUB AFRIQUE, LONDON E16 9HL.
Kiingilio ni paundi 15 za kule zaidi ya elfu 30 a kibongo na show itaanza saa nne usiku mpaka 12 asubuhi.....tehe itakuwa vangaaaaa i biliv..

TID & ALLY KIBA, halafu katikati kama Beny Kinyaiya...

TID AND ALI KIBA PERFORMING ON THE SAME STAGE ON THE 30TH OF APRIL 2010 @ CLUB AFRIQUE, LONDON E16 9HL. ENTRANCE 15 POUNDS FROM 10PM TO 6AM. KARIBUNI.

PREMIER YA LOVELY GAMBLE J5&MY DREAMS IN STORES THIS WEEK


LOVELY GAMBLE(MOVIE COVER)


Movie imetengenezwa na URBUN PULSE na imeshutiwa Uingereza,ndani kuna "galacha" wa filamu za kibongo ambaye ni kama alitushtua hv kwamba nasi tunaweza ishu hizi,anaitwa Steven Kanumba,naamini ni moja kati ya kazi za kitanzania ambazo hutakiwi kuzikosa aisii,sababu ziko kibao lakini mimi nakupa moja tu nzito ambayo sisi wadau wa haya mambo ya kuzitengeza hizi tunajua undani wake,ni kwamba imetengenezwa kwa muda mrefu(haijaripuliwa),nathubutu kusema imetumia mwaka mzima kutayarishwa mpaka kuletwa kwako,tofauti na zileeeeee za wiki mbili tayari eti unaambiwa iko dukani.Keshokutwa j5 pale club Billcanas inaoneshwa kwa mara ya kwanza(primiered).Ni Lovely Gamble itakayosambazwa na KAPICO TANZANIA Ltd.Usiikose.


MY DREAMS(MOVIE COVER)

Mzigo mwingine huu hapa wa "swahiba",unaitwa "My Dreams",huu utauona wiki hiihii kitaani kwako koz town nzima imeshachafuka na posters zake kali,umepigwa na RJ Company "vijana wa kazi"(sidhani hata kama huwa wanalala hawa jamaa) na unasambazwa na Steps Entertainment,nimeufuatilia sana mzigo huu katika hatua zote za utengenezwaji wake,naamini utakuwa NOMA sana,humo ndani macho yako yatamshuhudia Mahsein Awadh(Cheni),Rose Ndauka,Irene Uwoya(Mama Ndiku) na Vicent Kigosi(Ze dairekta),GRM wameshughulika,camera kabeba Razaq Ford na kwenye mashine "kaumiza mgongo"(editing) Ray mwenyewe,hebu fanyafanya kuutafuta.MY DREAMS.

This ishu kwa hisani ya bizzo 4 shizzo wa Ebony fm kupitia blog ya muziki na maisha.So chek nae kama vipi.

Monday, April 26, 2010

MISS KILIMANJARO KUFANYIKA JUNE

shindano la kumsaka Mrimwende wa kilimanjaro(Miss Kilimanjaro 2010) linatarajiwa kufanyika jume mwaka huu.Tayari warembo kutoka maeneo kadhaa mkoani Kilimanjaro wamekwishaanza mazoezi kujiandaa na shindano hilo.

Mdau wenu (mazimu) nilidodosadodosa kidogo nikataarifiwa kuna mrembo mmoja anatoka Chuo cha ushirika(MUCCOBS)...ah kumbe ni binti flan hivi namjua...Prisca...poa tutakuunga mkono na tutaunga mkono mshindi yeyote atakayepatikana.

Baadhi ya Warembo wakiwa katika pozi.

Hapa walikuwa Hotel ya Sal Salnero kwa ajili ya upigaji wa picha.

Hawa ni walimu wa warembo hao, ambao waliwahi kushiriki Umiss kwa vipindi tofauti.kulia ni Miss utalii kilimanjaro 2008, Elizabeth,Yuko Jacline pia mwenye red yeye alikuwa tatu bora Miss Kilimanjaro miaka mitatu iliyopita.

Priska, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Diploma wa Chuo cha Muccobs anawakilisha.jamani Muccobs tumpe sapoti binti huyu afanya kama alivyofanya Mwamini baada ya kutwaa taji la Miss Kilimanjaro mwaka jana.

Thanx mdau Busagaga kwa picha hizi.

CHAMBO AAGWA RASMI MUCCOBS-TUTAKUMISS BABA

Jana wanafunzi wa Chuo Kikuu kishiriki cha ushirika na Biashara MUCCOBS kupitia Serikali yao chini ya Rais Noel Katongo, iliandaa bonge la party kwa ajii ya kumuaga aliyekuwa mkuu wa chuo hicho, Prof Suleiman Chambo na kumkaribisha mkuu wa chuo mpya, Prof. Faustine Bee.

Party ilienda sawa, ikianzia pale Kilimanjaro Crane na kumalizikia kwenye ukumbi wa Nyerere uliopo katika Campus ya chuo hicho.Kabla ya hapo ilifanyika michezo kupitia mashindano ya Chambo cup ambapo upande wa basket, timu ya Cheti iliibuka vinara baada ya kuwabamiza degee mwaka wa pili kwa vikapu 55-50, wakati upande wa football mechi ya fainali ilivunjika baada ya dakika tisini wa kwanza na wa pili kutoka 0-0. Mwaka wa pili wakitaka zipigwe penati mwaka wa kwanza wanataka muda uongezwe hivyo...mpaka sasa mshindi kapuni labda tumuulize George Kusi(katibu wa wizara ya michezo) ama Waziri wake Mudi.

Basi bwana party ilikuwa hivi kipicha:

Sifuniiiiii where ar u broda? ilikuwa hivi usiku wa jana pale Kilimanjaro crane, hapa mtu mzima Yusuph Mazimu(mwandishi wa Blog hii) nilikuwepo pia na kampani kubwa ya bibie Hellen, one of the most beautiful lady in MUccobs.

Huyu ni bibie Kanakansia mmoja wa vigogo wa kamati ya maandalizi

Mwenekiti wa kamati ya maandalizi Kafui kushoto akiwa na Mkuu wa chuo mpya,Faustine Bee wakiteta jambo...labda anamwambia "mzee si unajua namaliza mwaka wa tatu sasa naomba nafasi ya yulee(Tuma)...tehe teh natania tu Tuma.

Ilikuwa na kumsosi kwenda mbele pale Kilimanjaro crane

Teh teh jamaa zangu,Dj Clever wa moshi fm na rodrick mushi mwandishi wa Tanzania Daima wakajitandikia msosi nje kwenye mlango wa kuingilia toilet, sikujua ama walikuwa wanatafuta appetite ya kula maeneo hayo ama ni basi tu waliamua

Tumaini Masuwe,teh teh mwalimu wangu yuko na rais wa kwanza wa serikali ya wanafunzi ya chuo hicho,(Nyerere wa Muccobs), Godfrey Maimu ambaye kwa sasa ni meneja wa M-pesa Kanda ya kaskazini.

Mr komba akiongoza meza bapa ya vigogo wa chuo cha ushirika

Hawa vijana walifanya kufuru mbaya,wanatokea chuo cha sanaa Bagamoyo walivunja

Jamaa nao walikuwemo, Eddwin wa channel 10,Enock(pole brother) na Kazukamwe

Hii ni Chambo's family, anaanza Prof. Chambo,mkewe Gladis Chambo,shemeji yake tumaini Mkami, kitinda mimba wake Jacline anayepiga darasa la sita na first born wake Sara anayemiliki masters, ambaye leo anasafiri kueleka Dar kwa ajili ya interview pale Ardhi university.All the best Sara....Na all the best baba Chambo hakika wanafunzi wa Muccobs tutakumiss sana.

Binafsi nisingeweza kuwa hapa nilipo bila mkono wake,Chambo nakumbuka wakati wa kufuatilia ishu za mikopo kwa diploma leavers waliojiungana degree, mh ilikuwa kasheshe mara vyeti vimefanya nini, mara flan sijui kaenda kule lakini ulisimamia vema na mambo yakaenda poa.
Tutakumiss profesa.

Sunday, April 25, 2010

SIMBA TUPENI RAHA WATANZANIA LEO


KIKOSI CHA SIMBA
Wekundu wa msimbazi simba leo hii wanaiwakilishA TANZANIA katika michuano ya kimataifa ya kombe la shirikisho kwa kuwakaribisha wamisri, Haras el hadoud kwenye uwanjawa taifa jijini dar es salaam.

Simba ndiyo timu pekee katika ukanda wa Afrika mashiriki iliyobaki kwenye mashindano ya kimataifa baada nyingine zote kuondolewa katika hatua za awali.

Simba haijawahi kufungwa katika ardhi ya tanzania na timu yoyote ya waarabu na pia inaingia uwanjani ikiwa ina rekodi ya kucheza michezo yote 22 ligi kuu Tanzania bara bila kufungwa na kumaliza mabingwa.
MUNGU IBARIKI SIMBA NA TANZANIA.

HUYU NDIYO ASHA NGEDERE ORIGINAL


Asha Ndedere Original na Tatu ukwaju wakiwa wanaenda shopping.Tehe teh yule Asha Ngedere wa TBC(Joti) ni feki tena China huyu ndiyo Original....Posa ruksa, Mahari hamna,,,karibuni wakware.

Salma Kijiko akiwa na shosty wake katika kutafuta vipodozi

Asha Ngedere feki Joti (kushoto)akiwa na Masanja Mkandamizaji

Friday, April 23, 2010

HELLEN AIBUKA KINARA MISS UNIVERSE


Helen Dausen,23.
Huyu ni binti kutoka Arusha, amewakilisha vilivyo kanda ya kaskazini kwa kuweza kuwagaragaza warembo wengine 19 walioshiriki shindano la Miss Universe mwaka huu lililofanyika mlimani city jijini dar es salaam usiku wa kuamkia leo.

Kama utani vile lakini ndo hivyo amelitwaa taji la Miss universe lililokuwa linashikiliwa na Iluminata James kutoka jijini Mwanza na sasa ataiwakilisha Tanzania katika shindano la Miss Universe la dunia. Binti huyu kwa taarifa yako wakati wenzake wameanza kambi huko dar es salaam, alikuwa jijini nairobi na Bizness zake, yeye pamoja na Moreen Bomba kutoka Morogoro ndiyo warembo pekee waliochelewa kuripoti kambini kati ya warembo 20 walioshiriki shindano hilo.Kwanini? Sijui....ndugu.

Katika kupamba shindano hilo, msanii wa kizazi kipya nameless alifunika mbaya kiburudani na kuonyesha anastanili kuwa gwiji wa muziki wa kisasa nchini Kenya na Afrika mashariki kwa ujumla.

Shindano la Miss Universe Tanzania lilianza rasmi mwaka 2007 ambapo mrembo Flaviana Matata aliibuka mshindi na kuiwakilisha Tanzania kwenye shindano la dunia la Miss Universe na kufuzu kutinga kwenye hatua ya 10 bora. Miss Universe Tanzania mwaka huu inadhaminiwa na Bia ya Serengeti, PSI, Precision Air , Hoteli ya Giraffe na ukumbi wa Mlimani City.

NAMELESS KUWASHA MOTO MISS UNIVERSE LEO

GWIJI la muziki kutoka nchini kenya,Nameless ni m moja kati ya wasanii lukuki watakaowasha moto leo kwenye ukumbi wa mliman city dar es salaam, kwenye shindani la kumsaka mrembo wa Miss universe mwaka huu.

Nyota wa muziki wa kisasa "Bongo Fleva kutoka Kenya Nameless (kulia) akiwa na Nyota Mwenzake wa Tanzania AY muda mfupi baada ya kuwasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam. Nemeless ni mmoja wa wasanii watako tumbuiza katika shindano la Miss Universe linalofanyika Aprili 23, 2010 katika ukumbi wa Mlimani City.

WENGINE WAWILI WATWAA TIKETI ZA COCA KWENDA SAUZ


Meneja mkuu wa Bonite, Gilbert Uisso akiwaasa watu kunywa soda ya coca,fanta na Srite ili kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo TV, Tshirt, soda ya bure na tiketi ya kwenda kushuhudia kombe la dunia.


Storiiiiiiii hiiii hapa: NA ISHU YA KUKABIDHI TIKETI IMEFANTIKA LEO MOSHI

MFANYAKAZI wa Benki ya NMB tawi la Ngaranaro mjini Arusha Mitabalulo Semuguruka ameibuka na tiketi ya Bure ya kwea Pipa na Coca cola kwenda kushughudia kombe la FIFA la Dunia nchini Afrika kusini kushughudia mechi ya Brazil na Portugal .
Mshindi mwingine ni Nelson Kundaeli mkazi wa majengo mjini hapa aliyejishindia tiketi ya Kwea Pipa na Coca Cola kwenda kushuhudia mechi hiyo wakati Emmy Mariki alijishindia televisheri aina ya Sony Bravia.
Meneja masoko wa kampuni ya kutengeneza vinywaji baridi jamii ya Coca Cola ya Bonite Bottlers ya mjini Moshi Gilbert Uisso aliwataja washindi wengine kuwa ni pamoja na Saidi Iddi kinyozi mkazi wa Soweto mjini Moshi ambaye amejinyakulia zawadi ya televisheni (TV).

Uisso alitoa wito kwa wateja wa kampuni hiyo kuendelea kunywa soda baridi jamii ya coca cola ambapo zawadi mbali mbali zikiwemo soda za bere,tshert,kofia,televisheni na tiketi za ndege kwa ajili ya kwenda kushughudia kombe la Fifa la Dunia nchini Afrika kusini mwezi Juni mwaka huu.

Akipokea tiketi yake Semuguruka ambaye ni mkazi wa Usa River mkoani Arusha alisema yeye ni shabiki wa tibu ya Livepool na Klabu ya Yanga na kwamba akiwa nchini Afrika kusini atashabikia timu ya Brazil kwa kuwa ni timu nzuri yenye kuinua vipaji vya wachezaji na nidhamu ya hali ya juu katika soka ulimwenguni.

Akipokea tiketi kwa niaba ya Nelson ,Katibu wa chama cha akiba na mikopo cha walimu wilaya ya Moshi vijijini Hubert Mariki akisema sasa ameamini na kufurahishwa na zawadi zinazotolewa na kampuni ya Bonite kuwa ni za kweli na katika sherehe zake zote ataweka vinywaji vya jamii ya coca cola.
‘Nitawafurahisha wageni wangu nyumbani kwa kunywa soda za Coca cola baridiii lakini vizibo vyote vitakuwa mali yangu’alisema Mariki huku akisisitiza wananchi kunywa soda hizo kwa wingi ili waweze kujishindia zawadi mbali mbali.

Mashuhuda wakishuhudia ugawaji wa tiketi kwa washindi uliofanyika kwenye kiwanda cha bonite Moshi.

Wednesday, April 21, 2010

TUTAKUMISS SANA GURU


Rapper huyu anayeheshimika sana amefariki dunia tar 19 asubuhi baada ya kuugua sana saratani na amekuwa akirudirudi kwenye koma mara kwa mara,akizungumza na vyombo vya habari jana jioni producer Solar amesema mchizi ameugua sana kwa takribani mwaka mzima na madaktari bingwa wamejitahidi sana kuokoa maisha yake lakini inaoneka kama MUNGU kampenda zaidi yetu,tutamkumbuka sana mchizi kwa ngoma kali,flows za ukweli na rylics za maana,"GURU umeondoka wewe lakini umetuachia ngoma zako kibao ambazo tutazitumia kukukumbuka".R.I.P.

Tuesday, April 20, 2010

MMOJA AFA, 19 HOI KWENYE AJALI MBAYA ILIYOTOKEA LEO WILAYANI MWANGA,

MTU mmoja amefariki dunia papohapo na wengine 19 kujeruhiwa vibaya baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori katika eneo la daraja la mto kifaru wilayani mwanga mkoani Kilimanjaro.

Ajali hiyo iliyolihusisha gari la Rombo Express lenye namba za usajili T255 AHV lililokuwa likitokea Rombo kwenda jijini Dar es salaam na Lori lenye namba za usajili T754 AEZ lililokuwa likitoke Hedaru wilayani Same kuja Moshi imetokea LEO majira ya saa mbili na nusu asubuhi.Kutokana na ajali hiyo magari yaliyokuwa yakielekea jijini Dar es salaa na Moshi yamelazimika kusimama na kusababisha foleni kubwa kwa muda wa masaa manne .

Akizungumza katika eneo la tukio kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Lucas Ng’hoboko alisema majeruhi wamelazwa katika hospitali ya Mawenzi na KCMC na kwamba aliyefariki ni fundi mitambo wa lori ambapo jina lake bado halijafahamika.

Kamanda Ng’hoboko alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa Lori ambalo lilikuwa limebeba mitambo ya kutengenezea barabara na kwamba uchunguzi unaendelea na pindi utakapokamilika sheria itachukua mkondo wake.

Basi la Rombo express likiwa chali kando ya barabara

mamia ya wakazi wa Kifaru wilayani mwanga wakishuhudia shughuli za uokoaji

Basi la Rombo express

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Lucas Ng'obhoko akizungumza na waandishi wa habari juu ya tukio hilo.

hili ni Lori lilogongana uso kwa uso na basi la Rombo express

Ilikuwa hatari, Poleni wafiwa, na majeruhi mungu atawaafu.AMEN


Ajali hiyo ilisababisha foleni kuuuubwa kwa takribani masaa manne