KOCHA wa klabu ya Stoke City inayoshiriki Ligi Kuu ya England, Tony Pulis, akiwa na baadhi ya wachezaji wa timu ya Zara Tours ya Moshi, wakiongozwa na Nasoro Chuji(mwenye kijani), mmoja wa nyota walioichezea timu ya daraja la kwanza ya Nyerere ya mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya "mapota"waliowapandisha kina Seeeman, wakiwa njiani kuelekea Kileleni mwa Mlima Kilimanjaro.
"Dole tupu", karibu chaiiiiiiiiiiiiiiii
Hili baridi noma..kama kule Himalaya!! Jamaa wamepozi kwenye moja ya sehemu za kupumzikia huko Mlimani.
Kocha wa Stoke,Pulis akikabidhi kikombe cha ubingwa wa kombe la Karibu fair, kwa nahodha wa timu ya Zara Tours ya Moshi,baada ya kuunyakuwa ubingwa huo katika mashindano ya mwaka jana yanayoshirikisha timu zinazowahusisha wafanyakazi wa sekta ya utalii hususani wanaoshiriki kuwapandisha watalii mlimani
Timu ya Zara Tours katika pozi pamoja na kipa wa zamani wa Arsenal, David Seeman(mwenye shirt nyeupe)mara baada ya kukabidhiwa kikombe na Pulis.
Hapo hamna zile pombe za kwetu.....naniii niii ni madude tu ya mbele Wisky,kompikax,...teh teh
Hawa jamaa zangu nao walijipenyeza kutandikwa picha na Kina Seema,kulia ni mwana Blog ya Busagaga.blogspot.com,Dixon Busagaga,Seeman,Hecton Chuwa,mwandishi wa magazeti ya Busness Times,Tony Pulis na mwakilishi wa Star TV na Radio free Afrika.
Eti hapa ndipo alipolala Seeeman......
Kastori kadogo haka hapa:
KOCHA wa klabu ya Stoke City inayoshiriki Ligi Kuu ya England, Tony Pulis, mchekeshaji maarufu katika runinga, Nick Hancock,na kipa wa zamani wa Arsenal na timu ya taifa ya Uingereza, wakiwa katika msafara wa watu 14 walitua nchini jumatano ya may 19 na kuanza kupanda Mlima Kilimanjaro siku hiyohiyo. Wakashuka Jumamosi usiku na kufikia katika Hotel ya Spring Land.
Safari yao ya kupanda mlima imewezeshwa na Kampuni ya Utalii ya Zara Tanzania Adventure, ambao waliwapandisha mlima, lakini lengo lao lilikuwa ni kuchangisha fedha kwa ajili ya kituo cha watoto cha Donna Louise Hospice cha nchini Uingereza.
Kwa mujibu wa Meneja wa Kampuni ya utalii ya Zara Tanzania Adventure, Yasin Mohamed Yasin, lengoni kuchangisha kiasi cha paundi 100,000 (sawa na dola 150,000) kwa ajili ya watoto hao. Kabla ya kuanza kupanda mlima huo, Pulis alisema licha ya kuwepo kwa vikwazo vidogo kama hali ya hewa.
Watu maarufu kutoka sehemu mbalimbali duniani wamekuwa wakipanda mlima huu na hii ni mara ya pili kwa wachezaji na viongozi wa soka kupanda mlima ambapo mapema Septemba mwaka jana bilionea wa Kirusi na mmiliki wa klabu ya Chelsea, Roman Abramovich alifanikiwa kupanda mlima huo na kuishia katika kituo cha barafu.
No comments:
Post a Comment