Sunday, May 9, 2010

HATMA YA UCHAGUZI MUCCOBS KESHO.


Kushoto ni mwenyekiti wa tume ya uchaguzi,MUCCOBS, Emanuel kafui, kulia ni mazimu(mwandishi wa blog hii) katikati ni wagombea watatu wa urais katika serikali ya chuo hicho,MUCSO, kutokea kulia ni Gudluk Julius, Rose mtei na Fredrick ngowi.

Hatma ya uchaguzi wa Rais wa serikali ya wanafunzi wa Chuo kikuu kishiriki cha ushirika na biashara, MUCSO, itajulikana kesho baada ya tume ya uchaguzi na uongozi wa Chuo hicho kukutana.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume hiyo, Bw. Emanuel Kafui mkutano huo wa kesho, utazingatia ushauri wa kisheria kujua hatua itakayofuata, baada ya kushindwa kupatikana kwa mshindi wa moja kwa moja, kutokana na idadi ya wapiga kura kutofikia robo tatu, kama katiba ya MUCSO inavyoeleza.

Hata hivyo Bw. Kafui amesema mchakato wa kumpata spika wa bunge unaendelea, huku matokeo ya wabunge ambayo hayaguswi na sheria ya robo tatu yangeanza kutolewa leo.

Uchaguzi huo huenda ukarudiwa baada ya wanafunzi 1526 kujitokeza kupiga kura kati ya 2218, ikiwa ni pungufu ya wanafunzi 138 wanaotakiwa kupiga kura kisheria ili kutimiza asilimia 75% ya idadi inayotakiwa inayotakiwa.

Bw. Amewataka wanafunzi wa chuo hicho kuwa wavumilivu wakati huu, ambapo tume na menejimenti ya chuo inaenda kukutana kuamua iwapo uchaguzi huo utarudiwa ama la.

No comments:

Post a Comment