Friday, June 11, 2010
DUNIA INAZIZIMA LEO...HUKO SOUTH
Rais wa kwanza wa Afrika kusini,Nelson mandela akishika kombe linaloanza kugombaniwa leo huko sauz. Afrika kusini vs Mexico wanafungua dimba jioni saa 11 leo.
Fainali hizi ni mara ya kwanza kuchezwa katika bara la afrika ingawa zipo baadhi ya timu za taifa kutoka afrika zikishiriki. Michuano hii itafunguliwa na raisi wa kwanza wa Afrika kusini na kushuhudiwa na viongozi wakubwa duniani kama Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Kin Moon. Makundi ambayo yanategemewa kukipiga tarehe kumi na moja mwezi huu kule Afrika kusini ni kama ifuatavyo;
Kundi A. Afrika Kusini, Mexico, Uruguay na Ufaransa.
Kundi B. Argentina, Nigeria, Korea Kusini na Ugiriki.
Kundi C. England, Marekani, Algeria na Slovenia.
Kundi D. Ujerumani, Australia, Serbia na Ghana.
Kundi E. Uholanzi, Denmark, Japan na Cameroon.
Kundi F. Italia, Paraguay, New Zealand na Slovakia.
Kundi G. Brazil, Korea Kaskazini, Ivory Coast na Ureno.
Kundi H. Hispania, Uswisi, Honduras na Chile.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment