Thursday, May 20, 2010

SISI WASANII TUNACHANGIA CCM, JE WEWE?


Juma Nature

Joh Makini

Chegge Chigunda

Chid Benzi

Prof Jay

Madee

Mwasiti

Barnaba

HAYA YANAWAKUTA WENZETU WALIO KARIBU NA MIGODI


Mama Otaigo wa kijiji cha Weigita,Mara.

Paul (8 year old boy) kutoka kijiji cha Nkerege,Mara.
Jaman kukaa karibu na Migodi kuna hasara zake na faida zake.... Ndugu yangu Chacha Benedict Wambura, mkurugenzi mtendaji wa Foundation HELP, anataka watanzania tufahamu haya.....Endelea.....

Dear Colleagues and partners,Greetings from North Mara in Tarime.I wish to share with you some photos of the current situation in North Mara. Rev. Magafu and I have been assessing and identifying the victims of the last year’s and ongoing waste ponds spillage at North Mara gold mine.
New cases of the victims are coming up with symptoms that are vivid and the situation is alarming. Two cases, though, needs immediate medical attention and action. This involves Mama Otaigo from Weigita village and Paul (8 year old boy) from Nkerege village.The situation we have found them in is far different from when we met them during the health screening done in January 7th 2010.
Their health state is deteriorating from day to day. I am attaching their current photos for your review.As the governments still remains silent on this matter attempts to get referral letters from government health facilities have proved abortive and therefore we need to act as soon as possible to save the lives of those who are critically ill.
An appeal is made to all of you to act in your different capacities.
Kind regards,Chacha.
=====================
Chacha Benedict WamburaExecutive DirectorFoundation HELPPlot No. 1, Block G. Old Custom Rd, LakeSide AreaP.O. Box 854 Musoma TanzaniaTel/Fax: +255 28 2620 575Cell: +255 787 945 414, +255 713 235 146Email: info@foundationhelp.org
Website: http://www.foundationhelp.org/

Monday, May 17, 2010

JAMANI UCHAGUZI RAIS MUCCOBS UTARUDIWA


Kuanzia kulia Emanuel Kafui(mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Mucso,wagombea wote watatu wa urais, Gudluck,Rose,na Fredrick pamoja na mwandishi wa blog hii...yusuph michael Mazimu(masanja jr.

Nimekuwa nikipata mails nyingi kuuliziwa nini matokeo ya uchaguzi wa Chuo cha Muccobs, especially watu waliokuwa nje ya Moshi..akiwemo ndugu yangu Sifuniel richard Mbaga(London).Ukweli ni kwamba matokeo ya ubunge yametoka...na mdau wenu(mazimu) nimefanikiwa kupata jimbo la pale Kibo(Mbunge)...asante kwa walionipigia Kura..ila upande wa urais kolamu ya wapiga kura haijatimia...ambapo inatakiwa 75% ya wanafunzi so uchaguzi huenda ukarudiwa....Thanx

FID Q KAANGUSHA DUDE JIPYA


Habari kutoka MJ Rec zinasema jumamosi walitarijia kuachia ngoma mpya ya Fid Q inayokwenda kwa jina la NGOSHA THE SWAGGA DON. MJ Rec ndiko ilikopikiwa na producer Marco Chali ambaye ijumaa aliweka wazi wamba ndio yupo kwenye hatua za mwisho mwisho kuimalizia.

RIP... THE BIG MAX


GODFREY BATESANYUKI MAXMILLIAN

Wadau wote wa blog hii,wanatoa pole nyingi kwa familia, ndugu na jamaa wa Max kutokana na kifo cha shujaa huyu aliyekuwa anasoma mwaka wa tatu(BA_AF) katika chuo kikuu kishiriki cha ushirika na biashara(MUCCOBS)... Amefariki dunia may 14/2010 kwenye Hospitali ya Muhimbili Dar es salaam baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu......Mungu aiweke roho ya marehemu Maxmahali pepa peponi ...AMEN

Monday, May 10, 2010

HONGERENI SANA MLISTAHILI KUWA MABINGWA


Chelsea FC jana ilitawazwa mabingwa wapya wa ligi kuu ya Uingereza baada ya kuibamiza Wigan mabao 8-0..
Drogba akiibuka mfungaji bora kwa mabao yake 29 ya msimu huu.


Chelsea FC

NDESAMBURO AONGOZA PSM MANAGERS PARTY.

Shemejiiiiiiiii.......Pauline Masalu akipokea cheti cha kumtambua kama member wa PSM Club toka kwa mgeni rasmi, mbunge wa Moshi mjini Philemon Ndesamburo katika bonge la party "PSM Managers Party" lilifofanyika wiki end hii@ Aventure Club moshi. Lilishirikisha wasomi wa chuo Kikuu Kishiriki cha ushirika na Biashara,MUCCOBS hususani wanaochukua fani ya procurement(ugavi).
Simon Kajiba na Hassan Shaqs" mwarabu mweusi" nao waliongoza kwa kuchafua meza.
Nassoro,Mjomba Abuu,Jackson Kileo na Yasin mashausi, nao walikuwemo.
Blog hii itaendesha utafiti kujua kama jamaa yangu huyu, Muba alilipa kiingilio ama mchango wa kufanikisha party hiyo... shaka hii ninayo cuz hakuwa free kabisa ukumbini hata pozi lake linajionyesha kama mtu anayeogopa kutolewa nje ya ukumbi saa yoyote vile.....lakini safiiiiiii.
Wajomba Simps akiwa na Abela pia mjomba mwingine Abuu Kilimba na ..... nao walivunja watakavyo...lakini mlilipia!!!!!!!!!!!!!!
Deodatus Msoka a.k.a Mpwa, huyu ni mjumbe wa tume ya uchaguzi, inasemekana alitoweka kabla ya kura hazijahesabiwa...kuwahi party....sijui lakini....kwa sababu ilikuwa the same day party inafanyika na uchaguzi wa rais wa Muccobs pia unafanyika.Pembeni yake ni Lydia ambaye alimpa kampani ya nguvu kweye party hiyo.
Rais wa PSM Club ya Muccobs, Deus Laurent akiwa na na Ida Pius kwenye pozi flan hivi.......so cool.

Photogenic Dafroza na Yasin Mashausi

Inawezekana alikuwepo pale Aventure Club kwa mambo mawili...kwanza ulinzi pili hii kitu aliypoishika...tehe tehe Lusaja Mwamponda aliwakilisha pia.

Lugano Mwambagi,katikati, mjumbe wa ukweli kwenye party hiyo, pamoja na MC Castory michael kulia na Boniface mchome.

Sina uhakika kama walialikwa, inawezekana walizamia...sijui lakini... kulia ni Frank a.ka ba Mishi akiwa na Sam ndani ya Nyumba.

Sunday, May 9, 2010

HATMA YA UCHAGUZI MUCCOBS KESHO.


Kushoto ni mwenyekiti wa tume ya uchaguzi,MUCCOBS, Emanuel kafui, kulia ni mazimu(mwandishi wa blog hii) katikati ni wagombea watatu wa urais katika serikali ya chuo hicho,MUCSO, kutokea kulia ni Gudluk Julius, Rose mtei na Fredrick ngowi.

Hatma ya uchaguzi wa Rais wa serikali ya wanafunzi wa Chuo kikuu kishiriki cha ushirika na biashara, MUCSO, itajulikana kesho baada ya tume ya uchaguzi na uongozi wa Chuo hicho kukutana.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume hiyo, Bw. Emanuel Kafui mkutano huo wa kesho, utazingatia ushauri wa kisheria kujua hatua itakayofuata, baada ya kushindwa kupatikana kwa mshindi wa moja kwa moja, kutokana na idadi ya wapiga kura kutofikia robo tatu, kama katiba ya MUCSO inavyoeleza.

Hata hivyo Bw. Kafui amesema mchakato wa kumpata spika wa bunge unaendelea, huku matokeo ya wabunge ambayo hayaguswi na sheria ya robo tatu yangeanza kutolewa leo.

Uchaguzi huo huenda ukarudiwa baada ya wanafunzi 1526 kujitokeza kupiga kura kati ya 2218, ikiwa ni pungufu ya wanafunzi 138 wanaotakiwa kupiga kura kisheria ili kutimiza asilimia 75% ya idadi inayotakiwa inayotakiwa.

Bw. Amewataka wanafunzi wa chuo hicho kuwa wavumilivu wakati huu, ambapo tume na menejimenti ya chuo inaenda kukutana kuamua iwapo uchaguzi huo utarudiwa ama la.

JOH MAKINI KUSHOOT VIDEO YA NGOMA YAKE MPYA KESHO


Mtu mzima Joh Makini kesho anatarajia kushoot video nyingine ya wimbo unaokwenda kwa jina la Haya aliofanya na mdogo wake Nikki wa Pili. Joh amesema shuting itakuwa mchana katika location tofauti tofauti.Video hiyo inatengenezwa na Visul Lab chini ya mtu mzima Adamu Juma.

Joh Makini akiwa na pamoja na wana

Exclusive SMS kutoka kwa AFANDE SELE.


“Watu wanapaswa kujua kwamba Watanzania ni walewale na si wajinga kama baadhi ya Ma-Dj na watangazaji wanavyofikiri kuwa kila wanachotaka wao basi Wabongo wataamini. Leo hii kuna artists wanapewa promo kila siku kwa kulazimisha lakini bado ukija huku mtaani watu bado hawawajui kwakuwa mchango wao katika game haufanani na sifa wanzopewa.
“Shabiki wa Afande, Prof. Jay, Daz Nundaz ndiyo huyo huyo atakayemkubali na artist mpya anayetoka vyema katika game, sasa kama kutoka kwa wasanii wapya dhaifu ndiyo kunasababisha kuwaua wakongwe wa ukweli, basi mashabiki hawatoendelea kuamini game na matokeo yake hadhi ya muziki inashuka.
Habari hii inaendele..ingia hapa ili kumalizia msg hii iliyotumwa na Afande Selle a.k.a Baba Tunda.
http://abdallahmrisho.blogspot.com/

TAIFA CUP.... KILIMANJARO YALALA KWA MARA


Mwita Kemoronge wa Mara akichanja mbuga kwenda kufunga mbele ya msitu wa mabeki wa Kilimanjaro, kwenye mchezo wa fungua dimba ya michuano ya Taifa cup , inayoendelea nchini kwenye vituo sita. Mchezo huu ulifanyika kwenye dimba la sheikh Amri Abeid karume na kushuhudia Kilimanjaro ikilala kwa mabao 2-3.

Friday, May 7, 2010

JAMANI TAFADHALINI MSIANGALIE ZILE PICHA TU!! NI ZA KWETU WATU WAZIMA


Wengi wanaonekana kutumia sana muda wao kuangalia "tirioz" kwenye net.

Godfrey Moshi maarufu kama Swala, mkimbiaji pekee aliyejipambanua MUCCOBS, akiwa na warembo Julieth Kimaro na Hamida Hamza wakikokochoa mtandanaoni... inaonyesha hapa Godi alikuwa akielekezwa namna ya kubonyeza vitufe vya Keybord...teh teh teh.

Tabasamu bint....Irene Kyata wakati ndiyo huuuu....usome sio kuangalia naniniii....blog ya mazimu11...

Baadhi ya wanafunzi "wakibrous" watakavyo,hawa ni CED sec yr.

Ni jambo zuri kwa uongozi wa Chuo Kikuu kishiriki cha ushirika na Biashara,MUCCOBS kilichoko Moshi, kuamua kutoa huduma ya Internet bure (wire less) kwa wanafunzi wake na wakufunzi wa chuo hicho, ni hatua nzuri itakayosaidia kuongeza muamko wa usomaji, upatikanaji wa material, na hata ujuzi zaidi wa masuala ya kuzama mtandaoni.... Safi sana... ombi langu..... uongozi wa Chuo hicho, wekeni pia Sehemu maalumu itakayokuwa na facilities za kutosha kama soketi ili huduma hiyo iwe kumpambaza inavyotakiwa lakini pia hata zile computer za kufundishia ziwezeshwe kuwa na huduma hii, ili kwa sisi tusiokuw ana laptop tujinome na mambo haya.... Otherwise mambo safiiii sana

I REALLY APRICIATE THIS GUMP PEA

Michael vs Neema
That's gud mdogo angu...ila buk mbele kwanza....Ila mkoa poa

ALLY KIBA KUWAKIBA WASWAHILI WA IRELAND


Ally Kiba yuko bize huko majuu, akiendelea na Bongo UK Spring Tour 2010, ambapo leo yuko Ireland anakamua kwenye ukumbi wa melody uliopo kwenye mji wa Dublin.
Show hii ni maalumu katika kuidhimisha miaka mitano ya usiku watu wa East Afrika maarufu kama"MOTO SANA" umoja unaosimamiwa na Dj Spaqz kutoka Kenya.

KUMBE BROTHER ANGU YUMO KWA KULISAKATA!!


Rais Kikwete,Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, waziri mkuu wa kenya,Raila Odinga, waziri mkuu mstaafu Salim Ahmed Salim wakirirudi Rhumba kukamilisha mkutano wa uchumi Duniani, katika viwanja vya Ikulu jijini dar es salaam.

Makamu wa rais,Dk. Ally Mohamed Shein akiyarudi na Bi. Elsie kanza kwenye kuhitimisha mkutano wa uchuni duniani.

'We ni noma'.....ilikuwa safi.. ukweli mkutano huu umekuwa na vitu vingi vya kujivunia.

WENGINE NANE WANYAKA TIKETI ZA KWEYA PIPA


Mmoja wa washindi wa tiketi akipewa mfano wa tiketi na mmoja wa vigogo wa Bonite bottles.

Baadhi ya vigogo wa Coca cola wakiwashuhudia utoaji wa tiketi za kweya pipa.
Gilbert Oisso , meneja wa bonite Bottles ya Moshi akitoa zake nasaha muda mfupi kabla ya kuanza kutoa zawadi za tiketi na TV kwa washindi wa promosheni ya kweya pipa na Cocacola.

Mzazi MT...Mtambalike mwenye glas, jamaa yupo PSM 3rd yr ndani ya MUCCOBS,mmoja wa wajumbe wa Chanel 10 ya Chuo cha Ushirika, alikuwepo kumpa kampani Mkubwa CEO wa Chanel 10,Edo....kuchukua tiketi yake ya Sauz pale Bomite.

Hawa ni washindi wa Tiketi za kweya pipa,wakiwa katika picha ya pamoja.

Wenzangu hawa ni washindi wa zawadi za TV
Katika tukio lililofanyika jana kwenye viwanja vya kiwanda cha Bonite, limeshuhudia watu sita wakiondoka na tiketi za kweya Pipa na wengine nane wakikwaa TV.
waliofanikiwa kunyaka Tiketi ni martha Bosco na Daniel Kessy kutokea Moshi,Nestroy Godfrey,Joseph Endry na Hermany Churson kutoka Arusha na Basil Joseph kutoka Singida. washindi hao wataungana na washindi wengine kufikisha idadi ya watu 200 kwenda Sauz kushuhudia mechi baina ya Brazil na Ureno ya Kombe la dunia itakayopigwa june 15 mwaka huu.

MUCCOBS WAPIGA KURA KUCHAGUA RAIS NA WABUNGE WAO


Mgombea urais, Gudluck julius akipiga kura... bila shaka kujichagua kuwa RAIS mpya wa MUCSO mwaka huu.

Rose Mtei,mgombea pekee mwanamke wa urais nae akijihukumu....kujiamulia hatma yake...bila shaka nae alijichagua.

Fredrick Ngowi"Pedeshee" akidondosha kura pia kujichagua...ni mgombea pekee wa urais toka mwaka wa kwanza.

Hawa ni mawakala wa wagombea urais wakishuhudiamambo yanavyokwenda kwenye chumba cha kupigia kura" TV Room yetu.

Kuanzia kulia Emanuel Kafui(mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Mucso,wagombea wote watatu wa urais, Gudluck,Rose,na Fredrick pamoja na mwandishi wa blog hii...yusuph michael Mazimu(masanja jr.), ambaye pia nilijipigia kura kujichagua kuwa mbunge wa jimbo la Kibo......

jamani tuchekiane kesho kwa matokeo ya kiukweli.... kujua nani kautwaaaaaaaaaaa nani kaukwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.......