Monday, April 19, 2010

YANGA ILIVYODODA KWA SIMBA JANA


Hassan Dalali, mwenyekiti wa Simba akipongezwa leo na mashabiki wa simba, kwenye ofisi za TFF baada ya kuwalaza yanga jana.

Wachezaji wa Simba wakifurahia kombe lao

Huyu hawatamsahau yanga, Mussa Hassan Mgosi wa kata ya Pasua mjini Moshi alifunga mabao mawili peke yana kuifanya simba kulaza yanga 4-3 na yeye kufikisha mabao 16 kwenye ligi , kwa mabao hayo dhahiri kiatu cha dhahabu kiko kwake.

Uhuru suleiman , mfungaji wa bao la kwanza la simba

Shadrack Nsajigwa akijaribu kuwahaada wachzeaji wa simba

Wachezaji wa yanga wakimlalamikia mwamuzi

mashabiki wa simba ilikuwa chereko kila kukicha

dah mdada huyu akaamua kumu sms jamaa yake...."me sipiki leo, ukale magengeni"

doh poleni sana,ni kama msiba vile, hapa ni baada ya Hilary Echessa kuifunguia simba bao la nne


waamuzi wa pambano la simba vs yanga,April 18/2010

Hongereni sanaaaaaaaaaaaaaaaaaana simba

WENGER AWALIWAZA MASHABIKI KWA CHAMAKH


Baada ya kupokea kipigo cha aibu kutoka kwa wigan jana, kocha wa arsenal, arsen wenger amewapoza mashabiki wa timu hiyo iliyokosa muelekeo kuwa Mmoroko Chamakh atatua Arsenal mara baada ya msimu kumalizika.

Friday, April 16, 2010

DAH NIMEWAMISS SANA JAMANI!


Shany J. mwakisombole.....maamaaaa nimekumiss sanaaa... u know wat si ndo nakupenda......teh teh rudi katika game bibie tumeimiss sauti yako nzitooooo.


Shany John Mwakisombole kushoto na Rebecca mgono "mkeiiii" enzi hizo wakiwa moshi fm, bila shaka ni kipindi cha midmorning cruz wanafanya hapa.....Shany alichapa mzigo VOT fm, sibuka fm na Kibo fm kabla ya kudondoka moshi fm.rebecca yeye anapiga kamsuli koko huko NAIROBI....

Kwao kitaa cha Nzega wanamuita Hassan wibonella lakini yeye kwa ujeuri wake ameamua kujiita Dee7...jamaa nilipiga nae mzigo VOT fm, na Sibuka fm lakini now anapiga mzigo Kiss fm mchek kwenye african beats jioni flan hiv. Dah broda nimemiss sana maneno yako ya "shombo' hewani na mtaani pia ,hope u r doing gwambaz huko Mwanza na Kiss fm. mshkaji anapenda sports sana, boxing, football na volleyball ila kucheza michezo hiyo, am nat sure kama anaweza sijawahi kumuona kwakweli.


Dula kulia akiwa na bint flan hivi Primilla Mosha ambaye ni shemeji yetu kwa mshkaji flan hiv(jina kapuni) shemejiiiiiiiii. Jamaa alikuwa PM wa Tripple A, VOT fm, Kili fm na Moshi fm, kashafanya makazi ya Mic katika maredio kibao, ofkoz radio one pia kakamua na hata RTD mnaiita TBC taifa siku hizi pia kapitisha voko zake...ukweli nimemiss msauti wako uliokufanya ukaitwa master voice.

Kulia ni Veronica Ollomi from kibosho, dah alikuwa PM na founder kwa upande wa kupitisha voko hewani pale Kili fm, buk kapiga St. Augustine huko mwanza, siku hizi mh anakula bata na shirika la KWIECCO. Kushoto ni Violeth Chonya "Lady VC" sauti yake inasikika Kili fm mpaka sasa....dah vero si ndo nimeimiis sauti yako katika mipashoooooooooo sasa si urejee tu kidogo katika game???
Renatus Kiluviaor Bizoo Manizo Bizzo 4 shizzo" Bwana wee, huyu jamaa ni fighter mbaaaya, producer yeye, presenter yeye, musician yeye, bisnessman yeye, blogger yeye...doh kila kitu, safi mzazi.Alikuwa Sibuka fm pale shinyanga kapiga sana kazi.Akapita Kili fm kidogo sasa nasikia mavituz anayapigia Ebony fm ya Iringa lakini yupo base ya dar es salaam. Mwana Nimemiss sana voko.

Kulia Halima Kasimu Yusuph Lema"HK kwao hapo juu tu...Machame, Kama unataka panda mlima Kilimanjaro...teh teh bint yuko safi..we msikilize kwenye show yake ya Lifestyle ndani ya kili fm-Kilimanjaro. Hapa nimejaribu kumkumbatia cuz nilikuwa nimemmiss mbaya...nilipomchek duh nikampa hug la kinyamwezi...nilipiga nae mzigo Kili fm kitambo ukweli sista ake namiss sana "kudeka kwako", now hata sina dada wa kunidekea, Jamila mwenyewe "Kauzu" labda Leyla pekee.
Hamza na Hamis, jamaa walipiga mzigo kibo fm, radio flan ambayo ilidumu hewani only 1 year mkoani kilimanjaro. Ilikuwa inapaishwa na madj hawa ambao pia walikuwa wanapitisha voko hewani kama kawa.tangu imepotea hewani kibo fm zaidi ya miaka miwili sasa sijasikia voko na scratching ukweli nimemiss sana izo ishu zenu brozas.

Thursday, April 15, 2010

MOSE RADIO&WEASEL TV WITH NEW ALBUM.

Ebwana waungwana hii ni kutoka kwa mdau wetu, mtu wangu ndugu yangu, kijana mwenzangu, tehe producer mwenz.... teh teh radio presenter mwenzangu anaitwa Bizzo Shizo Manizo...
Bizzo eeeeeh mwana nimekusoma ngoja niwasomeshe na wadau.... muzikinamaisha.... ama sio?

Mose Radio&Weasel Tv
Washkaji wanakula sana mashavu na si Kampala tu bali East Afrika na Ulimwengunikote kwa ujumla.Kwa mfano mwezi May mwaka huu wana show ya kufa mtu Washington DC na mara nyingi wanamuziki toka East Afrika wakipata shows za mbele,juu kwa juu wanapata pia shows zaidi na zaidi na zaidi.

Bebe Cool alikwishawahi kuwaponda hawa washkaji,akasema hawezi kutishika na watoto ambao hivi juzi kati alikuwa anawaona kwa macho yake mwenyewe wakiosha magari ya Jose Chamilion,lakini kiukweli mdau wangu tunapokuja kutazama ukali wa mwanamuziki au msanii fulani tunatazama kazi zake na wala si alichokuwa anafanya hapo kabla au sio??


Sasa sikia hii,washkaji wako tayari kurudi tena kwenu mashabiki na wanachoomba si kingine zaidi ya sapoti ya ukweli ambayo mmekuwa mkiionesha toka walipokuja kwa mara ya kwanza kabisa.

Wanakuja na mzigo "mupyaaa" soon,baada ya "Nakudata" ambayo ni albam yao ya kwanza kabisa na "Nyambura" ambayo ilifuata,sasa mzigo mpya uko tayari kabisa,kinachosubiriwa ni kupakuliwa na hiyo itakuwa baada ya show yao ya May huko Washington DC.Sasa hivi vijana hawa wanafanya vizuri na "ability".Mimi nawasubiri,wewe???

Wednesday, April 14, 2010

HII NIMEIKUTA KWENYE EMAIL YANGU NIKAONA WANDUGU NANYI MJIONEE


Huyu ni Nabii Titto.Nabii Titto yeye anahubiri matumizi ya pombe kwa kutumia Biblia,anasema kuwa mungu ameruhusu watu wanywe pombe kwani ni tiba sahihi kwa magonjwa mbalimbali .Alikuja ofisini kwangu ili nimsaidie kurekodi kanda na cd mbalimbali zitakazomafanya watu mbalimbali duniani kupata neno lake na kunisihi sana na kuniambia nikubali kwani ilo ndio ombi mungu alilomtuma kwangu.Mimi sikumkubalia ombi lake kwani ninavyoamini mimi na imani yangu ni vitu viwili tofauti.Je Wadau mnasemaje kuhusu Nabii Titto

jamani ndo hivyo


Tuesday, April 13, 2010

VAN IS BACK....ARSENAL HUREEEEEE

Jamani hii ni habari njema sana kwa mashabiki wa Arsenal, Robin van persie amerudi yuko fit
na Kocha wa Arsenal, Arsen wenger anasema yuko fit kuwavaa spurs Jumatano hii huko WHL
katika london derb itakayoamua hatma ya Arsenal msimu huu.
Hizi ni picha zilizopigwa leo akiwa mazoezini


van van van

teh teh van bwana

ee mungu asiumie huyu akawaumiza gunners


Karibu broda

ETI KUFA KUFAANA JAMANI!

Mara nyingi watanzania inapotokea ajali huwa tunawaza
namna ya kukwapua vitu , badala ya kusaidia ama kuokoa
majeruhi au mali zilizoathirika na ajali. hii ilinisikitisha sana
na ndo maana sikushangaa walivyofariki Morogoro kwenye
mlipuko wa mafuta,baada ya wakazi kulivamia gari la mafuta
lililoanguka.


Hapa walikuwa wanasubiri, mh walivyopata upenyo tu
wakavamia gari

mh jamani binadamu, hawafikirii uhai wao wanafikiria maisha yao tu.


Hili gari limeanguka,hawa jamaa hawakusubiri
waitwe walilivamia na kuanza chota mafuta,
doh hatari hii jamani.


Ilikuwa hekaheka kweli, eeh Mungu tusamehe

Monday, April 12, 2010

NDESA BWANA...CHEKI HII



Watoto hawa wanatoka kuchota maji nyumbani kwa mbunge wa Moshi mjini, Philemon Ndesamburo,jengo hilo pembeni lenye ukuta mweupe, maeneo ya mbokomu moshi. Nyuma yao wamama wakitoke home kwa mbunge huyo pia kuchita maji.Uhaba wa maji katika eneo hilo limekuwa historia baada ya mbunge huyo kuruhusu wakazi wa kitongoji hicho kuchota maji watakavyo na wapendavyo...ye si ana mtanki bwana that is why ishu zinakuwa ize.


Teh teh safi watoto..... but kuweni waangalifu

MVUA TABU TUPU MOSHI,BUT ASANTE MUNGU KWA MVUA HIZI

Mvua zinazoendelea kunyesha nchini, kwa baadhi ya maeneo ni faraja sana hasa huko kwetu kijijini, lakini mjini kwa kina Bite ni karaha tupu, cheki hapa ni eneo flan la moshi soweto....mji unaodhaniwa kuwa ni safi kuliko yote nchini ukiandaliwa pia kuwa JIJI.

Hii ni Soweto moshi maeneo flan ya Mawazo, utadhani wamepita watu wa rugbi?


Jamaa mwenye sepeto akijaribu kufukia baadhi ya mashimo, lakini sijui kama aliweza kumaliza.

Sunday, April 11, 2010

DENZEL WASHINGTON WA BONGO


Dar kama sio wewe, kumbe ni mwenzetu kutoka Mtaani kwetu..huyu ni KANUMBA WA MAMUVI YA KIBONGO akiwa mbele katika moja ya pilika pilika zake za kimuvi.

BONITE WAZIDI KUGAWA ZAWADI


Huyu alimchukulia mwanae Aman Makwao tiketi ya kwenda Sauz"


Mmoja wa washindi wa TV ,Teresia Massawe


Baadhi ya washiriki wa tukio hilo, Mbele ni Patrick Dereck wa Kili fm, Yusuph Mazimu (masanja Jr) wa Moshi fm na Bahati Mustapha wa Moshi fm wakipata ka-"tea" kidogo.


Vigogo wa Coca Kanda Bonite Moshi na Arusha wakijadiliana majambozi baada ya utoaji wa zawadi.

Saturday, April 10, 2010

WATATU WATWAA TIKETI ZA COCA KWENDA SAUZI

Kiwanda cha Bonite cha mjini Moshi leo kimetoa tiketi tatu kwa washindi waliobahatika kupata vizibo vya soda vyenye tiketi ya kwenda Sauzi kushuhudia kombe la dunia.

Pia imetoa zawadi za TV kwa washindi wengine sita. Waliopata tiketi za kwenda Sauz ni Saimon Makao wa Arusha, Aman Ole Mkwao mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar es salaam(UD) na Mohamed Bashiri wa kisongo Arusha. walitwaa TV aina ya sony ni Julius zephania wa KCMC moshi, Haji kileo wa Stand ya Mboya Moshi, Teresia Masawe wa Longuo KCMC, Jovina Samuel Mwita,Robinson elius na Kelvin Robert


Viongozi wa kiwanda cha bonite cha mjini Moshi, Kuanzia kushoto HRM, Bw.Dominic Urassa, General manager wa Arusha,Bw. Mongola Segule, Meneja wa fedha Bw. Gidion Kaaya, General manager wa Bonite Moshi,Gilbert Uisso na Christopher Loiruki ambaye ni meneja mauzo, wakiwa katika zoezi la kugawa tiketi kwa washindi wa kweya pipa na coca cola watakaokwenda kushuhuida kombe la dunia nchini Afrika kusini.


Hawa ni baadhi ya washindi wa tiketi pamoja na TV kwenye promosheni ya kweya pipa na Coca-cola.

Meneja mkuu wa Bonite, Gilbert Uisso akiwaasa watu kunywa soda ya coca,fanta na Srite ili kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo TV, Tshirt, soda ya bure na tiketi ya kwenda kushuhudia kombe la dunia.


Mshindi wa TV,julius Zephania akikabidhiwa zawadi yake na meneja mauzo wa Bonite, Christopher Loiruki.


Saimoni Makao mkazi wa Mianzini Arusha akipokea mfano wa tiketi yake kwenda sauz toka kwa meneja wa fedha Gidion Kaaya





Saimon akiwa na Yusuph M. Mazimu(masanja Jr), mara baada ya kukabidhiwa tiketi yake ya kwenda Sauz

Saimo akishukuru kwa kupata tiketi ya kwenda Sauzi.

Friday, April 9, 2010

Liyumba kizimbani tena leo


Aliyekuwa Mkurugezi wa fedha na utawala wa Benki kuu ya Tanzania (BOT), Amartus liyumba akiondoka kizimbani leo Kisutu dar es Salaam