Monday, May 10, 2010

NDESAMBURO AONGOZA PSM MANAGERS PARTY.

Shemejiiiiiiiii.......Pauline Masalu akipokea cheti cha kumtambua kama member wa PSM Club toka kwa mgeni rasmi, mbunge wa Moshi mjini Philemon Ndesamburo katika bonge la party "PSM Managers Party" lilifofanyika wiki end hii@ Aventure Club moshi. Lilishirikisha wasomi wa chuo Kikuu Kishiriki cha ushirika na Biashara,MUCCOBS hususani wanaochukua fani ya procurement(ugavi).
Simon Kajiba na Hassan Shaqs" mwarabu mweusi" nao waliongoza kwa kuchafua meza.
Nassoro,Mjomba Abuu,Jackson Kileo na Yasin mashausi, nao walikuwemo.
Blog hii itaendesha utafiti kujua kama jamaa yangu huyu, Muba alilipa kiingilio ama mchango wa kufanikisha party hiyo... shaka hii ninayo cuz hakuwa free kabisa ukumbini hata pozi lake linajionyesha kama mtu anayeogopa kutolewa nje ya ukumbi saa yoyote vile.....lakini safiiiiiii.
Wajomba Simps akiwa na Abela pia mjomba mwingine Abuu Kilimba na ..... nao walivunja watakavyo...lakini mlilipia!!!!!!!!!!!!!!
Deodatus Msoka a.k.a Mpwa, huyu ni mjumbe wa tume ya uchaguzi, inasemekana alitoweka kabla ya kura hazijahesabiwa...kuwahi party....sijui lakini....kwa sababu ilikuwa the same day party inafanyika na uchaguzi wa rais wa Muccobs pia unafanyika.Pembeni yake ni Lydia ambaye alimpa kampani ya nguvu kweye party hiyo.
Rais wa PSM Club ya Muccobs, Deus Laurent akiwa na na Ida Pius kwenye pozi flan hivi.......so cool.

Photogenic Dafroza na Yasin Mashausi

Inawezekana alikuwepo pale Aventure Club kwa mambo mawili...kwanza ulinzi pili hii kitu aliypoishika...tehe tehe Lusaja Mwamponda aliwakilisha pia.

Lugano Mwambagi,katikati, mjumbe wa ukweli kwenye party hiyo, pamoja na MC Castory michael kulia na Boniface mchome.

Sina uhakika kama walialikwa, inawezekana walizamia...sijui lakini... kulia ni Frank a.ka ba Mishi akiwa na Sam ndani ya Nyumba.

Sunday, May 9, 2010

HATMA YA UCHAGUZI MUCCOBS KESHO.


Kushoto ni mwenyekiti wa tume ya uchaguzi,MUCCOBS, Emanuel kafui, kulia ni mazimu(mwandishi wa blog hii) katikati ni wagombea watatu wa urais katika serikali ya chuo hicho,MUCSO, kutokea kulia ni Gudluk Julius, Rose mtei na Fredrick ngowi.

Hatma ya uchaguzi wa Rais wa serikali ya wanafunzi wa Chuo kikuu kishiriki cha ushirika na biashara, MUCSO, itajulikana kesho baada ya tume ya uchaguzi na uongozi wa Chuo hicho kukutana.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume hiyo, Bw. Emanuel Kafui mkutano huo wa kesho, utazingatia ushauri wa kisheria kujua hatua itakayofuata, baada ya kushindwa kupatikana kwa mshindi wa moja kwa moja, kutokana na idadi ya wapiga kura kutofikia robo tatu, kama katiba ya MUCSO inavyoeleza.

Hata hivyo Bw. Kafui amesema mchakato wa kumpata spika wa bunge unaendelea, huku matokeo ya wabunge ambayo hayaguswi na sheria ya robo tatu yangeanza kutolewa leo.

Uchaguzi huo huenda ukarudiwa baada ya wanafunzi 1526 kujitokeza kupiga kura kati ya 2218, ikiwa ni pungufu ya wanafunzi 138 wanaotakiwa kupiga kura kisheria ili kutimiza asilimia 75% ya idadi inayotakiwa inayotakiwa.

Bw. Amewataka wanafunzi wa chuo hicho kuwa wavumilivu wakati huu, ambapo tume na menejimenti ya chuo inaenda kukutana kuamua iwapo uchaguzi huo utarudiwa ama la.

JOH MAKINI KUSHOOT VIDEO YA NGOMA YAKE MPYA KESHO


Mtu mzima Joh Makini kesho anatarajia kushoot video nyingine ya wimbo unaokwenda kwa jina la Haya aliofanya na mdogo wake Nikki wa Pili. Joh amesema shuting itakuwa mchana katika location tofauti tofauti.Video hiyo inatengenezwa na Visul Lab chini ya mtu mzima Adamu Juma.

Joh Makini akiwa na pamoja na wana

Exclusive SMS kutoka kwa AFANDE SELE.


“Watu wanapaswa kujua kwamba Watanzania ni walewale na si wajinga kama baadhi ya Ma-Dj na watangazaji wanavyofikiri kuwa kila wanachotaka wao basi Wabongo wataamini. Leo hii kuna artists wanapewa promo kila siku kwa kulazimisha lakini bado ukija huku mtaani watu bado hawawajui kwakuwa mchango wao katika game haufanani na sifa wanzopewa.
“Shabiki wa Afande, Prof. Jay, Daz Nundaz ndiyo huyo huyo atakayemkubali na artist mpya anayetoka vyema katika game, sasa kama kutoka kwa wasanii wapya dhaifu ndiyo kunasababisha kuwaua wakongwe wa ukweli, basi mashabiki hawatoendelea kuamini game na matokeo yake hadhi ya muziki inashuka.
Habari hii inaendele..ingia hapa ili kumalizia msg hii iliyotumwa na Afande Selle a.k.a Baba Tunda.
http://abdallahmrisho.blogspot.com/

TAIFA CUP.... KILIMANJARO YALALA KWA MARA


Mwita Kemoronge wa Mara akichanja mbuga kwenda kufunga mbele ya msitu wa mabeki wa Kilimanjaro, kwenye mchezo wa fungua dimba ya michuano ya Taifa cup , inayoendelea nchini kwenye vituo sita. Mchezo huu ulifanyika kwenye dimba la sheikh Amri Abeid karume na kushuhudia Kilimanjaro ikilala kwa mabao 2-3.

Friday, May 7, 2010

JAMANI TAFADHALINI MSIANGALIE ZILE PICHA TU!! NI ZA KWETU WATU WAZIMA


Wengi wanaonekana kutumia sana muda wao kuangalia "tirioz" kwenye net.

Godfrey Moshi maarufu kama Swala, mkimbiaji pekee aliyejipambanua MUCCOBS, akiwa na warembo Julieth Kimaro na Hamida Hamza wakikokochoa mtandanaoni... inaonyesha hapa Godi alikuwa akielekezwa namna ya kubonyeza vitufe vya Keybord...teh teh teh.

Tabasamu bint....Irene Kyata wakati ndiyo huuuu....usome sio kuangalia naniniii....blog ya mazimu11...

Baadhi ya wanafunzi "wakibrous" watakavyo,hawa ni CED sec yr.

Ni jambo zuri kwa uongozi wa Chuo Kikuu kishiriki cha ushirika na Biashara,MUCCOBS kilichoko Moshi, kuamua kutoa huduma ya Internet bure (wire less) kwa wanafunzi wake na wakufunzi wa chuo hicho, ni hatua nzuri itakayosaidia kuongeza muamko wa usomaji, upatikanaji wa material, na hata ujuzi zaidi wa masuala ya kuzama mtandaoni.... Safi sana... ombi langu..... uongozi wa Chuo hicho, wekeni pia Sehemu maalumu itakayokuwa na facilities za kutosha kama soketi ili huduma hiyo iwe kumpambaza inavyotakiwa lakini pia hata zile computer za kufundishia ziwezeshwe kuwa na huduma hii, ili kwa sisi tusiokuw ana laptop tujinome na mambo haya.... Otherwise mambo safiiii sana

I REALLY APRICIATE THIS GUMP PEA

Michael vs Neema
That's gud mdogo angu...ila buk mbele kwanza....Ila mkoa poa

ALLY KIBA KUWAKIBA WASWAHILI WA IRELAND


Ally Kiba yuko bize huko majuu, akiendelea na Bongo UK Spring Tour 2010, ambapo leo yuko Ireland anakamua kwenye ukumbi wa melody uliopo kwenye mji wa Dublin.
Show hii ni maalumu katika kuidhimisha miaka mitano ya usiku watu wa East Afrika maarufu kama"MOTO SANA" umoja unaosimamiwa na Dj Spaqz kutoka Kenya.

KUMBE BROTHER ANGU YUMO KWA KULISAKATA!!


Rais Kikwete,Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, waziri mkuu wa kenya,Raila Odinga, waziri mkuu mstaafu Salim Ahmed Salim wakirirudi Rhumba kukamilisha mkutano wa uchumi Duniani, katika viwanja vya Ikulu jijini dar es salaam.

Makamu wa rais,Dk. Ally Mohamed Shein akiyarudi na Bi. Elsie kanza kwenye kuhitimisha mkutano wa uchuni duniani.

'We ni noma'.....ilikuwa safi.. ukweli mkutano huu umekuwa na vitu vingi vya kujivunia.

WENGINE NANE WANYAKA TIKETI ZA KWEYA PIPA


Mmoja wa washindi wa tiketi akipewa mfano wa tiketi na mmoja wa vigogo wa Bonite bottles.

Baadhi ya vigogo wa Coca cola wakiwashuhudia utoaji wa tiketi za kweya pipa.
Gilbert Oisso , meneja wa bonite Bottles ya Moshi akitoa zake nasaha muda mfupi kabla ya kuanza kutoa zawadi za tiketi na TV kwa washindi wa promosheni ya kweya pipa na Cocacola.

Mzazi MT...Mtambalike mwenye glas, jamaa yupo PSM 3rd yr ndani ya MUCCOBS,mmoja wa wajumbe wa Chanel 10 ya Chuo cha Ushirika, alikuwepo kumpa kampani Mkubwa CEO wa Chanel 10,Edo....kuchukua tiketi yake ya Sauz pale Bomite.

Hawa ni washindi wa Tiketi za kweya pipa,wakiwa katika picha ya pamoja.

Wenzangu hawa ni washindi wa zawadi za TV
Katika tukio lililofanyika jana kwenye viwanja vya kiwanda cha Bonite, limeshuhudia watu sita wakiondoka na tiketi za kweya Pipa na wengine nane wakikwaa TV.
waliofanikiwa kunyaka Tiketi ni martha Bosco na Daniel Kessy kutokea Moshi,Nestroy Godfrey,Joseph Endry na Hermany Churson kutoka Arusha na Basil Joseph kutoka Singida. washindi hao wataungana na washindi wengine kufikisha idadi ya watu 200 kwenda Sauz kushuhudia mechi baina ya Brazil na Ureno ya Kombe la dunia itakayopigwa june 15 mwaka huu.

MUCCOBS WAPIGA KURA KUCHAGUA RAIS NA WABUNGE WAO


Mgombea urais, Gudluck julius akipiga kura... bila shaka kujichagua kuwa RAIS mpya wa MUCSO mwaka huu.

Rose Mtei,mgombea pekee mwanamke wa urais nae akijihukumu....kujiamulia hatma yake...bila shaka nae alijichagua.

Fredrick Ngowi"Pedeshee" akidondosha kura pia kujichagua...ni mgombea pekee wa urais toka mwaka wa kwanza.

Hawa ni mawakala wa wagombea urais wakishuhudiamambo yanavyokwenda kwenye chumba cha kupigia kura" TV Room yetu.

Kuanzia kulia Emanuel Kafui(mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Mucso,wagombea wote watatu wa urais, Gudluck,Rose,na Fredrick pamoja na mwandishi wa blog hii...yusuph michael Mazimu(masanja jr.), ambaye pia nilijipigia kura kujichagua kuwa mbunge wa jimbo la Kibo......

jamani tuchekiane kesho kwa matokeo ya kiukweli.... kujua nani kautwaaaaaaaaaaa nani kaukwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.......

Thursday, May 6, 2010

MAZIKO YA WATOTO WATATU WALIOUAWA NA MAMA YAO MZAZI MJINI MOSHI

Paroko wa Parokia ya kristu mfalme ya kanisa katoliki jimbo la moshi,Padri Reginald Siipendi akiongoza maziko.
Mmoja wa watoto hao, tayari kuwekwa katika nyumba ya milele.
Mbunge wa viti maalumu, CHADEMA, Lucy Owenya akitoka kuweka udongo kaburini, kuaga miili ya marehemu hao.
Ilikuwa ngumu kwa wengine kuhimili hali halisi.Pole sana mama...Tuliwapenda watoto hawa ila Mungu kawapenda zaidi.
Mbunge wa Moshi mjini,Philemon Ndesamburo aliongoza mamia ya wakazi wa Moshi kwenye maziko hayo yaliyofanyika katikati ya wiki.

Watoto hao,Rose,Noela na Anthony walikutwa na mauti hayo April 29, baada ya kuuawa na mama yao mzazi,Benedikta Thadei, ambaye kwa sasa anatibiwa ugonjwa wa akili katika Hospitali ya Mawenzi chini ya ulinzi mkali wa jeshi la Polisi.
Kwa niaba ya wadau wa blog hii, napenda kutoa pole kwa wafiwa na wote walioguswa na vifo vya malaika hawa wa Mungu...Lakini pia naomba Radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza kwa picha ya watoto hao juu, lengo ni kuonyesha uhalisia na si vinginevyo......mazimu11.blogspot.com imejitahidi kuchagua picha hiyo moja kwa pembe nyingine ambayo angalau haionyeshi unyama uliofanyika.

Wednesday, May 5, 2010

UCHAGUZI WA RAIS NA WABUNGE WA MUCSO KUFANYIKA IJUMAA YA MAY 7 MUCCOBS


YUSUPH MICHAEL MAZIMU(mwandishi wa blog hii)...jamani nagombea pale bweni la kibo, plz naombeni sana kura zenu niweze kutumia uzoefu wangu wa kuongoza sehemu mbalimbali kuinufaisha jamii ya wana muccobs.

Bi. Rose hapa alikuwa nje ya Nyerere hall, MUCCOBS, akijiandaa kuingia kupiga kampeni

Bi. Rose wa pili kulia mgombea urais wa serikali ya wanafunzi katika chuo cha MUCCOBS, akiwa na mgombea mwenza Amani (mwenye tai) pamoja na wadau wengine.

Amani(kulia),Fredrick Ngowi mgombea urais, Pamoja na makamu wake, Mr. shani na wadau wengine, kwa mbaliiiiii namuona Novatus Massawe, kwao KCMC, eti mchaga wa mjini.

Mgombea urais,Fredrick Ngowi akiwa na

kulia ni Gogluck,mgombea urais kutoka BA-CED sec yr.

sehemu ya wanafunzi wakisikiliza sera za wagombea,aliyegeuka ni Miss kilimanjaro(2009) Mwamini,akiwa class pia kusikiza kinachoendelea kwa wagombea.

Baadhi ya wanafunzi wa mwaka wa tatu wakiwasikiliza wagombea wakinadi sera zao madarasani.huyu mweupe anayecheka ni mgombea wa urais katika uchaguzi wa mwaka jana, Abuu bila shaka anawacheka wenzake....hawajui kitakachowatokea....mh poa lakini.

Tuesday, May 4, 2010

HAPPY B'DAY!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!


Mwanadada Pennyl Mungilwa kutoka Channel 10 katika kipindi cha Extreem leo anakumbuka siku yake yakuzaliwa. Mungu akupe maisha marefu na yenye raha teleeeeeeeeeee, wala usikubali usichoke kwa kile kitu unachokitafuta hapa duniani ili uyafikie malengo yako

Mtu mzima DJ Venture kutoka Clouds FM na pia kila Jumamosi utampata pale Mzalendo PUB katika Fleva Night aliye katikati ya dada zetu naye anakumbuka siku yake yakuzaliwa, bro mimi sina la kusema zaidi ya kukuombea uishi maisha mazuri ili niendelee kupata mawazo yako yanayonifanya nisonge mbele hadi leo hii, much respect bro, ila kama kutakuwa na bata sehemu hebu nitonye ndugu yangu...
aaaah fresh tuu nitaibuka peke yangu

Monday, May 3, 2010

DROGBA AISOGEZEA KOMBE CHELSEA


Give me five men!!!!!Hawa walifunga bao moja kila mmoja na kuifanya chelsea kuibanjua liverpool 2-0 nyumbani kwao, Anfield. kwa ushindi huo, Chelsea inahitaji kushinda mechi yake ya mwisho dhidi ya Wigan ili kutwaa ubingwa wa ligi kuu Uingereza msimu huu.

Drogba akishangilia baada ya kuifungia chelsea bao la kuongoza kufuatia kuinasa pasi fyongo ya steven Gerald

CHID, PROF JAY NA BELLE9 KUWASHA MOTO MUCCOBS


Prof. Jay katika pozi tofauti.

May 8 mwaka huu, kutapigwa bash la nguvu" University Bash" pale club la liga mjini Moshi, ambapo prof Jay,Belle9,Matonya, na wasanii wengine wakali watafanya makamuzi ya nguvu, kuwaburudisha wanavyuo wa vyuo vikuu vya kanda ya Kaskazini.

Kiingilio ni Buku 10,000/= tu nahisi tutakutana pale wadau.....

WABONGO HAWATAKI KUMSIKIA TID HUKO LONDON


TID kushoto ,Beny na Ali Kiba

TID

TID akiwa jukwaani Club Afrique, London.

Unaambiwa Mwanamuziki TID ameboa watu sana huko london, kwenye show flan hivi ya wabongo ambapo alitupa mic kwa kisingizio kuwa Dj alikuwa kama anambania hivi,lakini mwenzake Ally kiba alikamua mbaya kila mmoja alienjoy, ilikuwa april 30 mwaka huu katika ukumbi wa CLUB AFRIQUE, LONDON E16 9HL.

Picha hizi na taarifa hii kantumia mdau wangu anaitwa sifuniel richard mbaga.......thanx brooo